• Login
    View Item 
    •   Repository
    • PhD. Theses and Dissertations
    • PhD Theses: Department of Department of Education and Social Sciences
    • View Item
    •   Repository
    • PhD. Theses and Dissertations
    • PhD Theses: Department of Department of Education and Social Sciences
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Usawiri wa Mwanasiasa wa Afrika Katika Ushairi wa Kiswahili

    Thumbnail
    View/Open
    Full Text Thesis (658.9Kb)
    Date
    2015-04
    Author
    Kinoti, Timothy M.
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Utafiti huu ulishughulikia usawiri wa mwanasiasa wa Afrika katika ushairi wa Kiswahili. Kimsingi, mtafiti alichunguza jinsi washairi mbalimbali walivyowasawiri wanasiasa wa Afrika kiubunifu kwa lengo la kudhihirisha walivyobadilika kisiasa na kimaadili kutoka enzi za ukoloni hadi kipindi cha siasa za vyama vingi. Utafiti huu ulichukulia kuwa wanasiasa hawa hutekeleza wajibu mkubwa katika maendeleo ya mataifa yao na bara la Afrika kwa jumla. Uafikiaji wa malengo mbalimbali ya maendeleo kama vile Ruwaza ya 2030 nchini Kenya na uimarishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kiasi kikubwa utategemea maamuzi ya kisiasa. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza nafasi ya ushairi wa Kiswahili katika uhifadhi wa historia ya mwanasiasa wa Afrika; kubainisha sifa za mwanasiasa wa Afrika kabla ya uhuru na kutathmini mabadiliko ya mwanasiasa wa Afrika baada ya uhuru kwa mujibu wa washairi wa Kiswahili. Mtafiti aliichukulia sauti ya mshairi kuwa sauti ya mwananchi ambaye ndiye huathiriwa na maamuzi na vitendo vya wanasiasa. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ulimbwende iliyoasisiwa na William Wordsworth na Samuel Taylor Coleridge na Nadharia ya Baada-Ukoloni ambayo inahusishwa na kazi za Edward W. Said, Gayatri Chakravorty Spivak na Homi K. Bhabha. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani ambapo mbinu ya sampuli ya kudhamiria ilitumiwa kuteua data kutoka kwa diwani teule. Uchanganuzi wa kimaelezo ulizingatiwa ambapo mashairi yaliyoteuliwa yalihakikiwa kwa mujibu wa madhumuni ya utafiti. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza imejumuisha utangulizi. Katika sura ya pili pana mwauo wa maandishi yanayohusiana na utafiti huu pamoja na misingi ya kinadharia. Sura ya tatu imeshughulikia mbinu za utafiti zilizotumiwa katika utafiti huu. Katika sura ya nne na tano, data imechanganuliwa, kuwasilishwa na matokeo kujadiliwa. Hatimaye, sura ya sita inatoa mahitimisho na mapendekezo kutokana na utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa ushairi wa Kiswahili ni utanzu wa fasihi ulio na umuhimu mkubwa katika kuhifadhi matukio mbalimbali ya kihistoria. Kupitia uhifadhi huu, sifa na vitendo vya mwanasiasa wa Afrika vimebainika katika vipindi mbalimbali vya kisiasa. Imebainika kuwa mwanasiasa wa Afrika aliyeonekana kuwa mzalendo kabla ya uhuru alibadilika ghafla uhuru ulipopatikana na kuwa mkandamizaji wa umma alioapa kulinda. Aidha, wanasiasa walioonekana kutetea upatikanaji wa demokrasia ya vyama vingi hawajatekeleza demokrasia hiyo. Licha ya dosari zilizobainishwa na utafiti huu, ni dhahiri kuwa bara la Afrika bado lina wanasiasa wachache vielelezo ambao wanaweza kuigwa na wanasiasa wa wakati huu na wale wa baadaye. Matokeo ya utafiti huu yatawanufaisha wasomi wa Kiswahili, waandishi na washikadau wote wa masuala ya kisiasa barani Afrika na kwingineko ulimwenguni.
    URI
    http://repository.embuni.ac.ke/handle/embuni/3402
    Collections
    • PhD Theses: Department of Department of Education and Social Sciences [12]

    University of Embu copyright ©  2021
    Contact us | Send Feedback
    Library ER 
    Atmire NV
     

     

    Browse

    All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    University of Embu copyright ©  2021
    Contact us | Send Feedback
    Library ER 
    Atmire NV